Hali si salama hivi sasa katika eneo la Bonde la Mkwajuni Kinondoni jijini Dar es salaam, na inaelezwa kuwa hali sio shwari kwani baadhi ya Wananchi wamechoma matairi pande zote za barabara na hakuna gari kupita. Jeshi la Polisi lipo eneo la tukio hivi sasa kukabiliana na tukio hilo ambalo chanzo chake unadaiwa ni baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa walikuwa wakazi wa eneo lililobomolewa ambao wameingia barabarani na kufanya fujo.
Kitendo hiki kimesimamaisha shughuli zingine ziliokuwa kuwa zikiendelea kwa muda. Ila mpaka sasa Jeshi la polisi linafanya jitihada za hali ya juu kukabiliana na swala hili.
SHARE TO
kujishindia mamilioni bonyeza hapo chini, ==>>

Post a Comment