Loading...

MISIRI YAENDELEZA MAUWAJI

video za wagombea urais bonyeza hapa chini

Wafuasi mbalimbali Misri
Watu wasiojulikana wamewaua waandamanaji 11 waliopiga kambi nje ya makao makuu ya Watawala wa Kijeshi Mjini Cairo,Misri.
Maafisa wanasema watu hao walianza kuwashambulia kwa mawe, mabomu na risasi waandamanaji hao ambao pia walijibu mashambulizi hayo. Wanajeshi pamoja na polisi wamezika makabiliano hayo, lakini baada ya saa sita za vurugu .
Kufuatia tukio hilo wagombea wawili wakuu wa Urais wamesimamisha kampeini zao kulalamikia mauaji hayo.
Abdul Moneim Aboul Fotouh,mgombea wa kujitegemea pamoja na kiongozi wa chama Freedom and Justice Party ambacho kinaungwa mkono na Muslim Brotherhood Mohammed Mursi wamelaani maafisa wa usalama kwa kuchelewa kuzuia fujo hizo.

Aidha chama cha FJP na kile cha Salafist Nour ambavyo vina wabunge wengi vimesusia mkutano na Baraza tawala la kijeshi{Scaf}.
Maandamano kulalamikia utawala wa kijeshi yameendelea tangu jeshi lichukue madaraka baada ya kuondolewa kwa Rais Hosni Mubarak Februari mwaka 2011.
Watawala wa Kijeshi wamelaumiwa kwa kuwakandamiza wapinzani na kuwaua waandamanaji pamoja na kuzima mashirka ya kiraia.
Watawala wa kijeshi hata hivyo wameahidi kuyakabidhi madaraka kwa raia mwishoni mwa mwezi Juni baada ya kufanyika uchaguzi wa Urais ambao wanasema utakuwa huru na haki

Mwanaharakati wa Uchina Chen Guangcheng
Mwanaharakati wa Uchina Chen Guangcheng amesema kuwa anahofia maisha yake na kwamba anataka kuondoka. Amesema hayo saa chache baada ya kuondoka hifadhi katika ubalozi wa Marekani.
Bw Chen amesema aliondoka kwenye ubalozi huo baada ya maafisa wa Uchina kutishia wanachama wa familia yake.
Lakini Marekani imesema haina habari zozote kuhusu vitisho hivyo na kwamba mwanaharakati huyo hakuomba hifadhi wakati wowote.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, yuko mjini Beijing kwa mazungumzo ya kibiashara na usalama na maafisa wa Uchina.
Awali, Bibi Clinton aliunga mkono Bwana Chen, ambaye amekuwa katika kifungo cha nyumbani kwa takriban miaka miwili.

haki za binadamu

Lakini wakati mazungumzo yalipoanza Bibi Clinton hakumtaja kwa jina.
''Marakeni inaamini kuwa hakuna nchi ina haki ya kumyima mtu haki ambayo ni haki ya kila binadamu- au kuadhibu mtu ambaye anatumia haki hizo. Bibi Clinton alisema.
Hapo Jumatano maafisa wa Uchina walishutumu Marekani kwa kuingilia maswala ya ndani ya nchi yao na kutaka Marekani iombe msamaha kwa kumhifadhi Bwana Chen katika ubalozi wao.
Mkutano unaofanyika Uchina ulitarajiwa kuzungumzia Syria na Korea ya kaskazini lakini imeghubikwa na mzozo wa kidplomasia juu ya Bwana Chen.
Bwana Chen amekuwa katika ubalozi wa Marekani kwa wiki moja baada ya kutoroka kutoka kifungo cha nyumbani katika kijiji chake kilichoko katika mkoa wa Mashariki cha Shandong


SHARE TO
kujishindia mamilioni bonyeza hapo chini, ==>>
Share/Bookmark International reporting trip.27 year old Missouri woman named Evelyn was recently featured on TLC's "My Strange Addiction", where she revealed that she's addicted to drinking air-freshner. According to Evelyn, she drinks 20 cans of air freshner a week and sprays up to 50 times daily.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSU HABARI HII

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KisimachaBurudani | Designed By KISIMA CHA BURUDANI
Back To Top