Mwandishi maarufu wa tamthilia na
kitabu cha ‘Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe’, Edwin Semzaba
amefariki juzi. Mbali na kuwa mwandishi maarufu,
Semzaba alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia, alikuwa
mwenyekiti wa Umoja Wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA).
Semzaba ambaye kitabu chake cha Ngoswe,
Penzi Kitovu cha Uzembe kilimpatia
umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, aliwahi kueleza kuwa alianza
kuandika kitabu hicho akiwa anasoma kidato cha pili akiwa na umri wa miaka 16
tu.
Aliimalizia kazi yake hiyo nzuri
baadae ambapo ilikubalika na kuanza kurushwa kupitia Radio Tanzania Dar es
Salaam (RTD) na baadae kuiweka katika kitabu kilichokubalika na kutumika kama
kitabu cha kiada kwa shule za sekondari.
Tovuti hii inapenda kuungana na
watanzania wote na wapenzi wote wa riwaya, hadithi na vitabu kutoa pole kwa
ndugu, jamaa, marafiki na taifa kwa ujumla. Apumzike kwa amani,Kisima cha Burudani kimetuma salamu za rambi rambi na kuwawakilisha wadau wake pia kwa pigo kubwa hili.
SHARE TO
kujishindia mamilioni bonyeza hapo chini, ==>>

Post a Comment