Jamhuri ya Sudan imekubaliana na
mpango wa Muungano wa Afrika (AU) wa kusitisha uhasama na Sudan Kusini, lakini
imesema itajilinda iwapo itashambuliwa.
Jumatano iliyopita, baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa, lilizipa nchi hizo mbili hadi Ijumaa kusitisha
mapigano, la sivyo ziwekewe vikwazo.
Lakini kumekuwa na ripoti za
kuongezeka kwa mapigano.
Sudan Kusini ilisema siku ya Alhamisi kuwa ndege za kivita za Sudan zilishambulia maeneo ya kijeshi katika jimbo la Unity. Sudan Kusini inasema pia ilishambuliwa ardhini.
Serikali ya Khartoum haijasema lolote kuhusu shutuma hizo.

mpango
wa AU
Kulingana na mpango wa amani wa Muungano wa
Afrika ambao nchi hizo mbili zimeridhia, Sudan na Sudan Kusini pia zitatarajiwa
kurudi katika meza ya mazungumzo, katika siku chache zijazo.Mzozo wa hivi karibuni ulianza mwezi uliopita wakati Sudan Kusini ilipodhibiti eneo linalozozaniwa lenye utajiri mkubwa wa mafuta la hejlig.
Japo Sudan ndio inayodhibiti eneo hilo kwa sasa, nchi hizo mbili bado zinaonekena kuwa huenda zikarejea vitani
SHARE TO
kujishindia mamilioni bonyeza hapo chini, ==>>

Post a Comment