Hapa ni Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili
wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere aliyefariki
nchini Marekani alikokuwa akitibiwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Mwili huo kesho utaagwa
nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Msasani kabla ya kusafirishwa kwenda
Butihama mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika keshokutwa.
Hili ndio gari maalumu ndugu walioandaa kwaajili ya kusafirisha mwili wa marehemu. Hapo ndio mwili wa marehemu ukiwekwa katika gari.
Huyu ndio mume wa marehemu akiwa katika majonzi makubwa. Nakufajiriwa na ndugu na majamaa walio hudhuria katika tukio hilo. Tukiwemo na kisima cha burudani kama ilivyo kawaida yetu.
Pembeni kushoto ni Kijana wa marehemu akiwa na ndugu wengine wakijadili mambo mawili matatu.
SHARE TO
kujishindia mamilioni bonyeza hapo chini, ==>>

Post a Comment