Ninalaani Vikali kitendo cha Waziri wa Michezo na Habari Nape Nnauye kulifungia gazeti la WAWIO kwa chuki zake binafsi bila ya kufikilia.
Tangu mwanzo nilipinga uteuzi wa magufuri zidi ya nape kuwa waziri kutokana na elimu yake kuwa ndogo na uwezo wa akili lakini pia kukurupuka bila kufikiria.
Nape Nnauye amelifungia gazeti la MAWIO bila kuweka sababu yoyote ni kwa nini amelifungia. Leo hii serikali ya Tanzania inapaswa kulilipa gazeti la mwanahalisi bilion 4 pesa za walipakodi kutokana na kufungiwa bila sababu Za msingi na serikali ya CCM ikiongozwa na kikwete.
kikwete na waziri wake walilifungia gazeti la mwanahalisi kwa chuki zao mwanahalisi wakashinda kesi leo hii serikali inapaswa kuilipa mwanahalisi bilion 4 huku waliosababisha hasara hii hawapo na ni wastaafu wala hawahusiki katika malipo hayo.
Nape kwa akili ile ile naye
anaenda kulifungia mawio kwa chuki zake mie nadhani ni muda wa bunge kutunga
sheria ambayo mtumishi yoyote akiitia hasara serikali akatwe mshahara wake na
mafao kufidia hasara hiyo kisha kufunguliwa mashtaka mahakamani hii inaweza
kuleta uwajibikaji,umakini kazini na kupunguza ulevi wa madaraka. Serikali inabidi kufikiria kwa makini na kuchukulia hatua swala hili.
SHARE TO
kujishindia mamilioni bonyeza hapo chini, ==>>

Post a Comment